Kurasa Muhimu

Sunday, November 23, 2014







CHAMA CHA WANAFUNZI WA KISWAHILI VYUO VIKUU VYA AFRIKA YA MASHARIKI (CHAWAKAMA)
OFISI YA KATIBU MKUU CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA
S.L.P. 351901 DAR ES SALAAM (TANZANIA)



 SIMU:  0777 445 569 (Mw/kiti)                                                                          
              0757 487 481 (Katibu)   

       Baruapepe: chawakama2014@yahoo.com                                                                                                                    


Kwa                                                                                                                           23/11/2014
Wanachama Wote wa CHAWAKAMA
Kanda ya Tanzania.
YAH:  TAARIFA YA MWALIKO WA KONGAMANO LA SABA (7) LA KITAIFA LA    
             KISWAHILI NA MKUTANO MKUU WA CHAWAKAMA.
Tafadhali shufu mada tajwa hapo juu.
Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHAWAKAMA Kanda ya Tanzania inayofuraha kuwataarifu Wanachama wote wa CHAWAKAMA katika kanda ya Tanzania kuwa kongamano la saba la Kitaifa la Kiswahili na Mkutano Mkuu wa CHAWAKAMA mwaka huu linatarajiwa kufanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia tarehe 23-25 Februari, 2015.

Hivyo basi, ninapenda kutumia fursa hii kuwaalika Wanachama wote kuhudhuria katika Kongamano hilo ambalo ni muendelezo wa makongamano ya Kitaifa ya CHAWAKAMA ya kila mwaka yanayofanyika kwa zamu katika Vyuo Wanachama.

Aidha napenda kutumia fursa hii kuwakumbusha viongozi wote wa matawi kutoa taarifa kwa walezi na uongozi wa Chuo ili kupata ruhusa ya kushiriki katika kongamano bila kuitilafiana na ratiba na taratibu za Chuo husika.

Nawatakia maandalizi mema ya kongamano.
Wenu katika kuienzi na kuikuza Lugha ya Kiswahili,
          ATHANAS BARNABA B.
Katibu Mkuu wa CHAWAKAMA Kanda ya Tanzania.
“KISWAHILI HAZINA YA AFRIKA KWA MAENDELEO ENDELEVU”







                                                                                           

No comments:

Post a Comment