Kuhusu Sisi


VIONGOZI WA CHAWAKAMA 2013/14

 

Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Vyuo vikuu Afrika Mashariki Tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam (CHAWAKAMA-UDSM ) zamani CHAKICHUKIDA ni miongoni mwa vyama vikongwe kabisa vya kitaaluma katika chuo kikuuu cha Dar es salaam. Chama hiki kilianzishwa mnamo mwaka 1972, wakati ambapo Chuo kikuu cha Dar es salaam kilikua bado kichanga kabisa. Hadi leo chama kina mafanikio mbalimbali kama vile kuzalisha na kukuza wataalam mbalimbali wa fani ya lugha za Kiswahili, isimu na fasihi na wengi wao ni Maprofesa, Madaktari wa falsafa na Wahadhiri wa Kiswahili katika vyuo mbalimbali duniani. Kwa hakika sitawataja kwa majina maana ni lukuki.
Baada ya kufanya shughuli mbalimbali ndani na nje ya chuo kikuuu cha Dar es salaam, Chama cha Kiswahili chuo kikuu cha Dar es salaam kimepata mafanikio makubwa kwa kuweza kushirikiana na Chama cha wahadhiri wa Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) katika uanzishwaji wa Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) mwaka 2004. Hivi sasa Chama kimeenea katika vyuo vikuu zaidi ya ishirini na tano Afrika Mashariki. Kwa mantiki hii Chuo Kikuu cha Dar es salaam ni tawi la CHAWAKAMA katika kanda ya Tanzania na tawi hili ndio makao makuu ya kanda chini ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kama mlezi wa kanda ya Tanzania. TATAKI pia ndio mlezi wa CHAWAKAMA-UDSM.

MALENGO YA CHAMA.
Chama kilianzishwa kwa malengo yafuatayo:
i.Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na na fasihi ya Kiswahili.
ii.Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya Kiswahili.
iii.  Kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
iv. Kuwaunganisha wanafunzi wa Afrika Mashariki na katika kukikuza Kiswahili.
v. Kushirikiana na vyama vingine vya Kiswahili katika  juhudi za kukiendeleza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama.
vi.Kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili ndani naje ya nchi kama vile BAKITA, TATAKI, TAKILUKI, UWAVITA, CHAKAMA, BAKIZA na nyiginezo.SAFU YA UONGOZI MPYA WA CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA

SN
JINA
WADHIFA
CHUO
NAMBA YA SIMU

1
MISSANA SANNE
MWENYEKITI
MUCE
0763-450604

2
EMMANUEL SANGA
M/MWENYEKITI
MAKUMIRA
0714-720844

3
MOSHI YUDA TADEI
KATIBU
DUCE
0765-565474

4

NAIBU KATIBU
SUZA


5
WILBERT EMMANUEL
MHAZINI MKUU
SEKOMU
0715-354640

6
MLAYA JUMA
MHAZINIMSAIDIZI
SAUT
0765-512783

7
BERNAD STEPHANO
MHARIRI MKUU
UOA
0754-568696

8
JACOB KINETI
MHARIRI MSAIDIZI
UDSM


9
TIMOTHY HEZRON
KATIBU MWENEZI
RUKO


10


TEKU


SAFU YA UONGOZI KWA UPANDE WA AFRIKA MASHARIKI – KUTOKA TANZANIA
SN
JINA
WADHIFA
CHUO
NAMBA YA SIMU

1
SAID GHANI
KATIBU MKUU
MUM
0712-851832

2
MGATA YOLANDA
MWEKA HAZINA MSAIDIZI
RUCO
0759-2204511 comment:

  1. Kwa maelezo yote kuhusu Tuzo ya Ushairi ya Ebrahim Hussein...

    https://www.facebook.com/pages/Ushairi/610865088994350

    ReplyDelete