MADA ZA KONGAMANO
KAULI MBIU YA KONGAMANO NI
“KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA
AFRIKA MASHARIKI”
Kauli
mbiu hii inalenga kuhimiza umoja na utangamano wa nchi za Afrika
Mashariki.Lugha ya Kiswahili ina mchango mkubwa sana katika kuleta
utangamano,umoja na mshikamano mwema baina ya nchi za Afrika Mashariki.Kando na
mchango wa Biashara,Michezo na
Elimu.Swali ni je,Lugha ya Kiswahili ina mchango wowote katika mchakato wa
kuimarisha na kukuza vipengele hivi vitatu; umoja,utangamano na mshikamano.
1.
Kiswahili ni lugha
mwafaka ya umoja wa Afrika mashariki.
2.
Nafasi ya lugha ya
Kiswahili katika tamaduni za nchi za Afrika Mashariki.
3.
Kiingereza au
Kiswahili? Katika mwamko mpya wa Afrika Mashariki huru.
4.
Kiswahili na michakato
ya kisiasa katika nchi za Afrika mashariki.
5.
Nafasi ya Kiswahili
katika sanaa ya kisasa (Karne ya ishirini na moja).
6.
Mchango wa lugha ya
Kiswahili katika upanuaji na uendelezaji wa elimu ya juu Afrika Mashariki.
7.
Kiswahili na
uimarishaji wa usalama katika ubia Afrika mashariki.
8.
Changamoto za kisiasa,kiuchumi
na kiusalama katika lugha ya Kiswahili,
9. Ubunifu
na talanta katika uzalishaji wa kazi mufti
ya fasihi ya Kiswahili
Lugha ya Kongamano: Lugha rasmi ya Kongamano ni Kiswahili. Makala
yaliyoandikwa kwa Kiingereza yatakubaliwa tu iwapo hapana budi.wajumbe
wanashauriwa kuanda makala yao katika lugha ya kiswahili
Ikisiri: Ikisiri za kati ya maneno 200-300 zitumwe kabla ya tarehe 30 Mei 2014 kwa Mratibu wa Kamati ya Maandalizi kupitia barua meme
kwenye anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com,AU Mhariri Mkuu godwinalex664@yahoo.com
(+255718252853) au kwa
katibu mkuu wa chawakama Afrika mashariki Ahamadi Jumbe. Chawakama.am@gmail.com .
Makala: Makala
kamili ya ikisiri zitakazokubaliwa yatumwe kwa Mratibu kwa baruameme kufikia
tarehe 30 Juni 2014 kupitia anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com
Ili kupata nafasi ya kuwasilisha makala uliyoandaa ni
lazima.mjumbe atume ikisiri na hatimaye makala kamili ya mada aliyoandaa.Makala
haya yatachapishwa katika chapisho la makala la kongamano kabla ya tarehe 15 Julai 2014 .utaratibu na mpangilio
wa uwasilishaji utatolewa tarehe 30
Julai 2014.