Kurasa Muhimu

Thursday, May 15, 2014


MADA ZA KONGAMANO

KAULI MBIU YA KONGAMANO NI
“KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI”

Kauli mbiu hii inalenga kuhimiza umoja na utangamano wa nchi za Afrika Mashariki.Lugha ya Kiswahili ina mchango mkubwa sana katika kuleta utangamano,umoja na mshikamano mwema baina ya nchi za Afrika Mashariki.Kando na mchango wa  Biashara,Michezo na Elimu.Swali ni je,Lugha ya Kiswahili ina mchango wowote katika mchakato wa kuimarisha na kukuza vipengele hivi vitatu; umoja,utangamano na mshikamano.

1.      Kiswahili ni lugha mwafaka ya umoja wa Afrika mashariki.
2.      Nafasi ya lugha ya Kiswahili katika tamaduni za nchi za Afrika Mashariki.
3.      Kiingereza au Kiswahili? Katika mwamko mpya wa Afrika Mashariki huru.
4.      Kiswahili na michakato ya kisiasa katika nchi za Afrika mashariki.
5.      Nafasi ya Kiswahili katika sanaa ya kisasa (Karne ya ishirini na moja).
6.      Mchango wa lugha ya Kiswahili katika upanuaji na uendelezaji wa elimu ya juu Afrika Mashariki.
7.      Kiswahili na uimarishaji wa usalama katika ubia Afrika mashariki.
8.      Changamoto za kisiasa,kiuchumi na kiusalama katika lugha ya Kiswahili,
9.      Ubunifu na talanta katika uzalishaji wa kazi mufti  ya fasihi ya Kiswahili
Lugha  ya Kongamano: Lugha rasmi ya Kongamano ni Kiswahili. Makala yaliyoandikwa kwa Kiingereza yatakubaliwa tu iwapo hapana budi.wajumbe wanashauriwa kuanda makala yao katika lugha ya kiswahili
Ikisiri: Ikisiri za kati ya maneno 200-300 zitumwe  kabla ya tarehe 30 Mei 2014 kwa Mratibu wa Kamati ya Maandalizi kupitia barua meme kwenye anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com,AU Mhariri Mkuu godwinalex664@yahoo.com (+255718252853) au kwa katibu mkuu wa chawakama Afrika mashariki Ahamadi Jumbe. Chawakama.am@gmail.com .
Makala: Makala kamili ya ikisiri zitakazokubaliwa yatumwe kwa Mratibu kwa baruameme kufikia tarehe 30 Juni  2014 kupitia anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com

Ili kupata nafasi ya kuwasilisha makala uliyoandaa ni lazima.mjumbe atume ikisiri na hatimaye makala kamili ya mada aliyoandaa.Makala haya yatachapishwa katika chapisho la makala la kongamano kabla ya tarehe 15 Julai 2014 .utaratibu na mpangilio wa uwasilishaji utatolewa tarehe 30 Julai 2014.

No comments:

Post a Comment