Wahitimu wa CHAWAKAMA-CKDSM 2014 wakiwa katika picha pamoja na Mkurugenzi wa TATAKI Dr. Mosha ambaye pia ni Mlezi wa chama, baada ya kutunukiwa vyeti vyao vya uanachama.
Saturday, June 14, 2014
Thursday, May 15, 2014
MADA ZA KONGAMANO
KAULI MBIU YA KONGAMANO NI
“KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA
AFRIKA MASHARIKI”
Kauli
mbiu hii inalenga kuhimiza umoja na utangamano wa nchi za Afrika
Mashariki.Lugha ya Kiswahili ina mchango mkubwa sana katika kuleta
utangamano,umoja na mshikamano mwema baina ya nchi za Afrika Mashariki.Kando na
mchango wa Biashara,Michezo na
Elimu.Swali ni je,Lugha ya Kiswahili ina mchango wowote katika mchakato wa
kuimarisha na kukuza vipengele hivi vitatu; umoja,utangamano na mshikamano.
1.
Kiswahili ni lugha
mwafaka ya umoja wa Afrika mashariki.
2.
Nafasi ya lugha ya
Kiswahili katika tamaduni za nchi za Afrika Mashariki.
3.
Kiingereza au
Kiswahili? Katika mwamko mpya wa Afrika Mashariki huru.
4.
Kiswahili na michakato
ya kisiasa katika nchi za Afrika mashariki.
5.
Nafasi ya Kiswahili
katika sanaa ya kisasa (Karne ya ishirini na moja).
6.
Mchango wa lugha ya
Kiswahili katika upanuaji na uendelezaji wa elimu ya juu Afrika Mashariki.
7.
Kiswahili na
uimarishaji wa usalama katika ubia Afrika mashariki.
8.
Changamoto za kisiasa,kiuchumi
na kiusalama katika lugha ya Kiswahili,
9. Ubunifu
na talanta katika uzalishaji wa kazi mufti
ya fasihi ya Kiswahili
Lugha ya Kongamano: Lugha rasmi ya Kongamano ni Kiswahili. Makala
yaliyoandikwa kwa Kiingereza yatakubaliwa tu iwapo hapana budi.wajumbe
wanashauriwa kuanda makala yao katika lugha ya kiswahili
Ikisiri: Ikisiri za kati ya maneno 200-300 zitumwe kabla ya tarehe 30 Mei 2014 kwa Mratibu wa Kamati ya Maandalizi kupitia barua meme
kwenye anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com,AU Mhariri Mkuu godwinalex664@yahoo.com
(+255718252853) au kwa
katibu mkuu wa chawakama Afrika mashariki Ahamadi Jumbe. Chawakama.am@gmail.com .
Makala: Makala
kamili ya ikisiri zitakazokubaliwa yatumwe kwa Mratibu kwa baruameme kufikia
tarehe 30 Juni 2014 kupitia anwani ifuatayo: Billysakwa@gmail.com
Ili kupata nafasi ya kuwasilisha makala uliyoandaa ni
lazima.mjumbe atume ikisiri na hatimaye makala kamili ya mada aliyoandaa.Makala
haya yatachapishwa katika chapisho la makala la kongamano kabla ya tarehe 15 Julai 2014 .utaratibu na mpangilio
wa uwasilishaji utatolewa tarehe 30
Julai 2014.
TANGAZO TANGAZO TANGAZO.
UONGOZI WA CHAWAKAMA TAWI LA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM UNAPENDA KUWATANGAZIA WANACHAMA NA WADAU WOTE WA LUGHA ADHIMU YA KISWAHILI KWAMBA KUTAKUWA NA KONGAMANO LA KUMI LA KIMATAIFA.
KONGAMANO HILO LITAFANYIKA NCHINI KENYA KATIKA CHUO KIKUU CHA LAIKIPIA KUANZIA TAREHE 21/ 08/2014 MPAKA TAREHE 24/08/2014. WASHIRIKI WA KONGAMANO WATATOKA KATIKA KANDA ZOTE AMBAZO NI WANACHAMA WA CHAMA HIKI AMBAZO NI TANZANIA, KENYA, UGANDA,RWANDA, BURUNDI NA KONGO.
MADA MBALIMBALI ZINAZOHUSU LUGHA YA KISWAHILI ZITAWASILISHWA NA KUJADILIWA KATIKA KONGAMANO HILO, AMBAZO ZINAGUSA SANA SUALA LA UMOJA NA USHIKAMANO MIONGONI MWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI.
KAULI MBIU.
KAULIMBIU ITAKAYOLIONGOZA KONGAMANO HILO NI:
KISWAHILI MALIGHAFI YA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI.
GHARAMA.
- KILA MSHIRIKI ANAPASWA KUTOA FEDHA TASLIMU KIASI CHA SHILINGI ELFU HAMSINI NA TANO (55,000/=) ZA KITANZANIA KWA AJILI YA CHAKULA, MALAZI, FULANA NA CHETI CHA USHIRIKI. FEDHA HIYO ITAKUSANYWA KABLA ILI IWASILISHWE KWA VIONGOZI HUSIKA KWA AJILI YA MAANDALIZI YA KONGAMANO.
- KILA MSHIRIKI ATAPASWA KUJITEGEMEA KWA GHARAMA ZA USAFIRI WA KWENDA NA KURUDI, NA KUAANDAA HATI YA KUSAFIRIA. KWA SASA VIONGOZI WAPO KWENYE MCHAKATO WA KUWAANDIKISHA WOTE WATAKAOPENDA KUSHIRIKI, ILI ZOEZI LA KUANDAA HATI ZA KUSAFIRIA LIANZE MARA. HIVYO, NI VYEMA UKAJIANDIKISHA SASA KWA VIONGOZI AMBAO WANAHAMASISHA KATIKA MIHADHARA MBALIMBALI. KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA VINGOZI KWA NAMBA ZIFUATAZO.
MWENYEKITI 0757487481
KATIBU 0757794239
MHAZINI 0655832600
MHARIRI 0769978920
Friday, April 4, 2014
TANBIHI: PICHA HIZI NI MIONGONI MWA MATUKIO YALIYOJIRI KATIKA KONGAMANO LA CHAWAKAMA KANDA YA TANZANIA LILILOFANYIKA KATIKA CHUO CHA ECKERNFORDE-TANGA FEBRUARI 2014.
Subscribe to:
Posts (Atom)